MAMBO yameiva, kikosi cha TP Mazembe kitaingia nchini Jumatano ya Januari 27, 2021 , siku ambayo yanaanza mashindano mafupi ya Simba Super Cup, maalumu kwa ajili ya kuiandaa klabu ya Wanamsimbazi na Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kupitia kwa mtendaji mkuu wa klabu hiyo, Barbara Gonzalez walitangaza kuwepo kwa mashindano hayo, yatakayowasaidia kuwaandaa wachezaji wao kwa ligi ya ndani na ya Mabingwa Afrika.
Katika ukurasa wao wa mtandao wa kijamii (Instagramu), Simba iliandika kikosi kamili cha TP Mazembe kitakachokuja kushiriki mashindano kwamba kitaongozwa na mkongwe Tresor Mabi Mputu na Mtanzania anayeichezea klabu hiyo, Thomas Ulimwengu.
Kikosi hicho kimeundwa na wachezaji ambao ni Sylvain Gbohou, Patou Kabangu, Maukoro Bosso, Mputu Mabi Tresor, Thomas Ulimwengu, Moustapha Kouyate, Koffi Kouyate, Bakula Ulonde, Martial Zemba Ikoung.
Wengine ni Mayombo Etienne, Ochaya Benson, Mwape Tandi, Kalaba Rainfor, Kabaso Chngo, Okito Kazidi Nicolas, Gmasengo Yumba Godet, Bossou Nzali Adam, Kisangala Boba, Sudi Bibonge, Tshibangu Isaac, Joel Freddy Kaougi, Bedi Guy Stephane, Binemo Madi Le Beau na Arsene Zola Kiaku.
Simba imezialika timu mbili katika mashindano hayo ambazo ni TP Mazembe itakayocheza Julai 29 na Al Hilal mwalikwa wa pili na Julai 31 dhidi ya wenyeji Simba.