Wachezaji wa nne wa klabu ya Palmas ya nchini Brazil pamoja na rais wa timu hiyo wamefariki dunia katika ajali ya ndege siku ya Jumapili.

Ndege hiyo ndogo ilibeba wachezaji hao wachache kwaajili ya kuwapeleka kwenye mchezo wao siku ya Jumapili na kupata ajali huku ikiarifiwa hakuna aliyenusurika.
Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinadai kuwa Rais Lucas Meira pamoja na wachezaji wake Lucas Praxedes, Guilherme Noe, Ranule na Marcus Molinari wote wamefariki.
”Ndege ilizima ghafla na kupata ajali mwisho mwa barabara Tocantinense Aviation Association. Tunasikitika kuripoti hakuna aliyenusurika.”
Rubani wa ndege hiyo aliyefahamika kwa jina la Wagner pia ni miongoni mwa waliofariki kwenye ajali hiyo.