Walijua kwamba ndio yuko mwaka wa pili kama kocha tangu alipojiunga na klabu hiyo kwahiyo, kungekuwa na wakati angekumbana na changamoto.
Huu ndio wakati kama huo huku katika mechi ya Jumamosi, akipata bao 1 kwa nunge dhidi ya Fulham ikiwa ni ushindi wao wa pili katika mechi saba ilizoshiriki kwenye Ligi ya Premier.
Jumanne walikutana na Leicester City ambayo iko katika iko nafasi ya tatu katika jedwali la Ligi kuu ambao wako alama sita mbele ya Blues
Wakati Lampard aliojiunga na timu hiyo, hakukuwa na matarajio yoyote. Alikuwa na kikosi kidogo, alikuwa amempoteza mchezaji Eden Hazard na pia kulikuwa na marufuku ya uhamisho. Angeweza tu kufanyakazi na kundi la wachezaji aliokuwa nao pekee.
Na sasa ili aweze kushindana vilivyo, walihitajika kuwekeza pesa zaidi katika kupata wachezaji wazuri. Lampard amefanya hivyo – na sasa hivi bila shaka kuna mtazamo mwingine.
Wakati unapopewa pesa kwa ajili ya jambo fulani, kinachotarajiwa ni matokeo mazuri. Lakini matokeo yanayolengwa huwa hayatokei haraka kama ilivyo matumaini ya wengi.
Kuna ulazima wa kuwa mvumilivu, amini mtu ambaye unajua ataleta matokeo chanya yanayosubiriwa.
Wakati kocha wa Manchester City Pep Guardiola alipojiunga nao, alitumia pesa nyingi lakini hakushinda katika msimu wote wa kwanza. Hii inaonesha kwamba inachukua muda kuongeza thamani kwa kitu chochote kile.
Wachezaji ambao wameletwa na Lampard ni vijana wadogo kutoka nje ya nchi na wanahitaji muda kuzoea Ligi ya Premier na pia sasa hivi kuna ugonjwa wa corona.
Umekuwa mwaka mgumu kwa karibu kila mmoja na hilo inawezekana limeathiri matokeo ya mechi ya timu huku wengine wakiwa wagonjwa, hawawezi kuona rafiki zao na pia hawawezi kuona familia zao yaani mazingira yamekuwa magumu kweli.
Ukizingatia yote hayo, nafikiri watu wanatoa matamshi makali kwa Lampard.
Pia, Lampard hajakuwa na wakati wa kuhusisha wachezaji wote wapya na kuwapa muda wa kuzoeana na timu kwasababu alikuwa na muda kidogo kabla ya msimu.