Kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil anatarajiwa kujiunga na klabu ya Uturuki Fenerbahce.
Mchezaji huyo aliyeishindia kombe la dunia timu ya Ujerumani anajiunga na nyota wa Taifa Stars Mbwana Samatta ambaye alijiunga na klabu hiyo kwa mkopo kutoka Aston Villa.
Fenerbahce pia ilisema kwamba wamekubaliana kandarasi ya miaka minne na mchezaji huyo wa Tanzania mwenye umri wa miaka 28 ambaye itatiwa saini mwisho wa mkopo huo.
Samatta ambaye ndiye mshambuliaji nyota wa klabu hiyo sasa anatarajiwa kucheka na wavu mara kwa mara kutokana na pasi murua zitakazojiri kutoka kwa Ozil iwapo atasajiliwa rasmi na klabu hiyo
Samatta alijiunga na Villa mwezi Januari mwaka uliopita kutoka klabu ya Ubelgiji ya Genk
Wakati huohuo Ozil alisafiri hadi nchini Uturuki siku ya Jumapili ili kufanyiwa vipimo ili kukamilisha mkataba huo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 bado amesalia na nusu msimu katika kandarasi yake ya Arsenal lakini aliwaaga wachezaji wenzake katika uwanja wa mazoezi wa timu hiyo kabla ya kuondoka.
Ozil hajaichezea Arsenal tangu timu hiyo ilipopata ushindi wa 1-0 dhidi ya West Ham mnamo mwezi Machi na amekuwa hachezeshwi na mkufunzi Mikel Arteta.
Alijiunga na klabu hiyo katika uhamisho wa dau la £42.4m kutoka Real Madrid mwaka 2013 na aliwasaidia kushinda kombe la FA mara tatu.
Katika mahojiano na runinga ya Uturuki ya NTV siku ya Jumapili , Ozil alisema kwamba anafurahia kujiunga na Fenerbahce na kwamba atavalia fulana ya timu hiyo kwa majivuno. ".
Vyombo vya habari vya Uturuki mapema mwezi huu vilidai kwamba Fenerbahce itamsaini Ozil mwezi Januari.
Na alipoulizwa kuhusu mkufunzi Arteta, alisema kwamba uhamisho utafanyika kama ndio suluhu bora kwa kila mtu. ".
Ozil alizaliwa nchini Ujerumani lakini ana mizizi ya Uturuki na mwenyekiti wa Fenerbahce Ali Koc amesema kwamba kumsajili Ozil ni ndoto njema ".
Mwaka 2019 mabingwa hao mara 19 wa kombe la ligi ya Uturuki walipinga uhamisho wa Ozil kutokana na sababu za kiuchumi.
Klabu hiyo ya Instanbul imekabiliwa na tatizo la kifedha katika miaka ya hivi karibuni hali iliofanya klabu ya Istanbul Basaksehir kushinda taji lao la kwanza la ligi Julai iliopita.
Ozil alizungumza kuhusu jinsi anavyoipenda klabu hiyo wakati wa masuali aliokuwa akiulizwa katika mtandao wiki iliopita.
''Fenerbahce ni kama Real Madrid nchini Uhispania, Klabu kubwa nchini humo''.
Baada ya kuanzishwa mechi 10 Arteta alipoajiriwa mwezi Disemba 2019, Ozil hajachezeshwa tena tangu soka ianze baada ya wimbi la kwanza la virusi vya corona mwezi Juni.
Ijapokuwa Ozil alisema msimu wa majira ya joto uliopita kwamba atasalia na Arsenal hadi siku yake ya mwisho ya kandarasi yake mwezi Juni 2021, Arteta alimwacha nje katika kikosi cha Yuropa League na kile cha ligi ya Premier.
Alikuwa mchezaji anayelipwa fedha nyingi katika historia ya klabu hiyo mnamo mwezi Januari 2018, lakini akakataa kupunguziwa mshahara wake wakati wa majira ya joto bila mechi kuchezwa huku Arsenal ikihitaji kudhibiti matumizi yake.