03 Mar 2021 00:00:00 AM Breaking News
Mukoko amtia Kaze lawamani YangaTetetesi za soka Ulaya Jumanne 09.02.2021: Messi, Lukaku, Ings, Konate, Shoretire, Alaba, ElliottGomez: Tulieni, tupo tayari kwa vitaVikwazo vya kiuchumi Iran havitaondolewaMangungu kuanza na mambo 11 SimbaMastaa Yanga wapewa siku sabaMorrison azidisha utamu SimbaMbunge akumbusha kilio cha Katiba MpyaKaze afunguka ishu ya Yanga kufungiwa kusajiliTanzania Kutopewa Chanjo ya Corona na WHOGomes amtega Mkude SimbaMikataba yote ilioafikiwa siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho UlayaUGANDA: Watu 32 wapoteza maishaKesi ya Iran kuhusu Marekani yasikilizwaChikwende, Lwanga kuonja balaa la Ligi KuuKambi Yanga Dar kibokoTetesi za soka Ulaya Jumatano 03.02.2021: Messi, Neymar, Mbappe, Sancho, Alli, HakimiPisi Kali Ligi Kuu WanawakeBilionea wa Amazon Jeff Bezos ajiuzuluMTV wameingia kwenye 18 za Diamond tena"Kazi ya serikali sio kulisha Watu"- Rais MagufuliMmemsikia Kaze..! kwa mafundi hawa kazi mnayoCristiano Ronaldo achunguzwa kwa kusafiri ili kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mpenzi wake licha ya masharti ya coronaAjali ya treni na Lori la mizigo VingungutiSimba yabeba taji laoWaandamana kupinga sheria ya usalama wa taifa, UfaransaMAGUFULI: Daktari Aliekimbia Hospitali ya Serikali Kwenda Binafsi AfutweRC Mbeya aunda tume kuchunguza kifo cha derevaGomes: Simba yangu... Mtakula nyingiii!Mastaa Yanga tumbo jotoMagufuli "Wivu unavyowakwamisha watanzania"Mamilioni Yanga yaitesa SimbaMkurugenzi WHO kukutana na Mawaziri wa AfrikaNidhamu ya kujilinda imeitoa Stars Waziri Bashungwa: Tutawasaidia Wasafi Tv kufunguliwaMan United kuchuana dhidi ya Arsenal, Everton na Southampton baada ya kulazwa na Sheffield UnitedRais Yoweri Museveni 'Sitaki Kupatanishwa na Wapinzani'Tamko la Rais Magufuli kuhusu magonjwa ya mlipukoHuko Yanga kumekuchaRais Magufuli Awapa Siku 7 Waziri Gwajima na Jafo, Kisa Hichi HapaMorrison ang'ara, Simba ikiua WasudanSerikali Yapiga Marufuku Kuchukua Ardhi Bila Kulipa FidiaKauli ya Farid Musa baada ya kuibeba Taifa Stars “Guinea kazi wanayo” (+video)Serikali kufutia leseni kwa wanaopandisha bei ya mafuta ya kupikiaWallace Karia Apitishwa na FIFATetesi za soka Ulaya Jumatano 27.02.2021: Di Maria, Upamecano, Garcia, Zirkzee, Tarkowski, BentekeAkamatwa Austria na vinyonga 74 kutoka TanzaniaWaziri Mpango: Chukueni Tahadhari Dhidi ya CoronaBarbara: Tulitaka kuialika Yanga Super Cup lakini...Biden aanza na rais wa Urusi: Putin usituingilie hayakuhusuKwa mara ya kwanza mwislamu achaguliwa kama mwanasheria mkuu MarekaniSimba, Al Hilal kamili Super CupRais Magufuli kuzindua shamba la Miti ChatoBiden: Marufuku raia wa Afrika kusini kuingia MarekaniBruno Fernandes: "Iwapo nimechoka, ninapofikia umri wa miaka 30 au 32, sitoweza kucheza''Rais Xi Jinping aonya dhidi ya kuanzisha vita vipya baridiLokosa is RedThe Hammers, hatahivyo wanakabiliwa na ushindani wa kumsajili Lingard, ambaye pia amehusishwa na Aston Villa na Sheffield United. (Express)Trump atuhumiwa kwa kuchochea uasiTetesi za soka Ulaya Jumanne 26.01.2021: Dzeko, Lingard, Alli, Draxler, Mustafi, Veron, GrayBobi Wine ana siku nne za kupinga matokeo mahakamaniJPM Aanika Alichozungumza na Rais wa EthiopiaChelsea imekataa ofa ya West Ham ya kumchukua mlinzi wa Italia, 26, Emerson Palmieri kwa mkopo. (Sunday Mirror)Kikosi kizima TP Mazembe chaanikwa, kutua J5Rais wa Mexico apata maambukizi ya COVID-19BAHANUZI: Maisha yangu Mungu anajuaAjali ya ndege yaua wachezaji wanne na rais wa klabu BrazilTetesi za soka Ulaya Jumatatu 25.01.2021: Odegaard, Lingard, Gilmour, Mbappe, Alaba, ModricMliosambaza Stika za TRA jiandaeni kisaikolojiaMtambo wa mabao Jamie Vardy kufanyiwa operesheniKimbunga Eloise chapiga Msumbiji na kuleta mafurikoUrusi yaishutumu Marekani kwa kuingilia mambo yake ya ndaniKaze aanza na gia mpyaDidier Gomes kocha mpya SimbaLady Jay Dee Awafungukia Wanaopenda Nyimbo za MatusiMwanamuziki Shetta Aachana na MkeweSarpong Abakishwa Kwa Masharti Mazito YangaRC Kunenge apokea msaada wa mifuko 800 ya sarujiMarekani, WHO sasa mambo safiTaifa Stars yakabidhiwa Milioni 60, kila la heri michuano ya CHAN 2021Waziri Mkuu Mongolia ajiuzuluJohn Bocco karudi kuokoa jahazi la Taifa Stars CHAN Viongozi wa Ulaya kutafuta muarubaini wa Corona leoNMB yajipanga kusaidia na kufufuliwa zao la Mkonge nchiniMkude: Simba naombeni msamahaChameleone ashindwa uchaguzi wa umeyaFiston aongeza mzuka Yanga, kuwasili JumamosiTanzia: Mbunge wa CCM Afariki DuniaMajaliwa atoa maagizo haya kwa Wizara ya KilimoRais mpya wa Marekani Joe Biden aanza kazi baada ya kuapishwaKwanini Lampard anastahili muda zaidi Chelsea?Mexico inataka ushirikiano wa Biden kumaliza mgogoro wa wahamiaji mpakaniTanzia: Naibu Kamishna Magereza Afariki DuniaShikhalo: Simba SC itatoboa AfrikaBiden kuapishwa leo, machozi yamtoka kaburini kwa mtoto wake Alichokisema Rais Magufuli Kuhusu Ajira Milioni 8Simba yanasa mbadala wa Mkude MaliBalozi wa Marekani Uganda azuiwa kumuona Bobi WineMarekani! Taharuki ya Mlipuko Eneo la Uapisho wa Joe Biden, Zoezi LaahirishwaOle Gunnar Solskjaer atumia mfano wa Mlima Kilimanjaro kuhamasisha wachezajiPolisi Uganda yathibitisha kumuweka kizuizi cha nyumbani Bobi WineMesut Ozil: Kiungo wa kati wa Arsenal kujiunga na Samatta klabu ya FenerbahceTuisila awatikisa nyota MsimbaziUchaguzi Uganda 2021: Upi mustakabali wa Bobi Wine baada ya kushindwa uchaguzi?Bobi Wine kukimbilia mahakamani kupinga matokeo ya uchaguziChikwende, Mnigeria wamesaini Simba, Morrison mh!Rais Magufuli: Shule ipo Dar Es Salaam wanafunzi wanakaa chini, Mkuu wa Wilaya yupo, Mkuu wa Mkoa yupo, Mkurugenzi wa Ubungo bado anakusanya kodi yupo na Mbunge wa Ubunge yupo tena ni profesa wa Elimu.Jinsi uapisho wa Joe Biden utakavyokuwa tofauti huku ulinzi ukiwa mkali?

Tuisila awatikisa nyota Msimbazi

tuisila pic

KUTOKANA na kasi aliyonayo winga wa Yanga, Mkongomani Tuisila Kisinda ‘TK Master’ zimemtikisa beki wa zamani wa kimataifa wa Simba, Boniface Pawasa aliyeamua kutoa mchongo kwa mabeki wa timu pinzani kuweza kumdhibiti na kuondokana na presha kubwa.

Tuisila aliyesajiliwa msimu huu kutoka AS Vita ya DR Congo, amekuwa akisifika kwa kasi kubwa na hasa kuwapora mipira na kuwatoka mabeki, ikiwamo kitendo alichomfanyia beki wa Simba, Joash Onyango katika Kariakoo Derby na kusababisha kumchezea faulo iliyozaa penalti.

Penalti hiyo ilitumiwa vyema na Yanga kujipatia bao lao kupita Michael Sarpong kabla ya beki huyo kutoka Kenya kusahihisha makosa kwa kufunga bao la kusawazisha dakika za lala salama na kufanya matokeo ya mchezo huo uliopigwa Novemba kumalizika kwa sare ya 1-1.

Hata hivyo, kwa uzoefu alionao katika nafasi ya beki, Pawasa aliiambia Mwanaspoti amekuwa akimfuatilia winga huyo wa Yanga na kubaini mbinu ambazo mabeki wa timu nyingine wanaweza kuzitumia ili kumdhibibiti uwanjani.

Pawasa alikiri Tuisila ni mchezaji hatari ambaye hatakiwi kupewa nafasi ya kumiliki na kuvuta mpira kisha kugeuka na kuanza kukimbia nao, badala yake mabeki wacheze kwa kumkaba mtu kwa mtu.

Alisema Tuisila ni mchezaji anayetumia akili kubwa, kwamba akimaliza jambo lake la kuwapa presha mabeki, kisha anaanza kutembea kama vile hayupo uwanjani, kitu alichokigundua kinawasahaulisha mabeki wasijue anavuta pumzi ya kuweka mwili wake upya kwa ajili ya kuwasumbua zaidi.

“Tuisila hatakiwi kupewa nafasi, beki namba mbili na beki wa kati ndio wanapaswa kuwasiliana namna ya kumkabili, ndipo wanaweza wakapunguza makali yake, kwani si mchezaji ambaye anaingia ndani ya eneo la penalti, huwa anakimbilia pembeni hiyo ndio nafuu yao, lasivyo angekuwa anawaliza mara kwa mara,” alisema Pawasa ambaye kwa sasa ni kocha na kuongeza;

“Tuisila hafikii mbio alizokuwa nazo Said Maulid ‘SMG’ wakati wa kumkaba, tukiona mpira umepigwa kwake, mmoja anabaki nyuma, mwingine anaenda kukabana naye bila kumwachia nafasi, mbaya zaidi alikuwa anamlazimisha beki amfanyie makosa ndani ya eneo la penalti, ndio maana jina lake lina nguvu hadi leo, kitu ambacho Tuisila anakikosa.”

Alimshauri Kocha Cedric Kaze kumuongezea maarifa Kisinda kwamba anapokokota mipira awe anaangukia ndani ya eneo la penalti na sio nje, ili kushinda mbinu za mabeki wajanja wanaokuwa wanamvutia nje na timu kuishia kupata faulo ambazo ni mara chache wakafunga.

“Laiti Tuisila angekuwa ananyanyua macho yake kuona anaenda wapi angekuwa hatari zaidi, pia awe anaangukia ndani ya eneo la penalti na sio anavyofanya kutumia nguvu nyingi, wakati mwingine haziifaidishi timu, ila ni mchezaji mzuri sana anayetakiwa kuonge-zewa maarifa kidogo sana,” alisema.

Naye nyota wa zamani wa Simba, aliyewahi kuzinoa timu kadhaa nchini ikiwamo Kagera Sugar, Njombe Jiji na Lipuli ya Iringa, Mrage Kabange, alisema Tuisilada ni mchezaji anayetakiwa beki asilale pindi anapokuwa na mpira, kisha asimruhusu aukokote mbele yake.