Licha ya kukiri kibano cha kufungiwa kusajili kwa vipindi vitatu kitakuwa na athari kiufundi kwenye kikosi chake, kocha Cedric Kaze amesema Yanga haitakuwa timu ya kwanza au ya mwisho kukumbana na adhabu hiyo.
Jana taarifa ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) ilieleza kuipa Yanga adhabu hiyo kwa kushindwa kumlipa aliyewahi kuwa mshambuliaji wake, Amiss Tambwe.
Tambwe raia wa Burundi aliishitaki Yanga Fifa akitaka alipwe malimbikizo ya mshahara wake baada ya kuachana na klabu hiyo miaka kadhaa iliyopita.
Kaze afunguka ishu ya Yanga kufungiwa kusajili
