WADAU wa soka siku hizi wameanza kuvutiwa na Ligi Kuu ya Wanawake huku na kule kumbe ni kwa sababu ya kuwatazama warembo wanavyojua kusakata soka. Sio Ulaya tu ambako ‘pisi kali’ zimekuwa zikipagawisha mashabiki.
Kwenye Ligi Kuu ya Ufaransa alikuwepo mrembo aliyeitwa Kosovare Asllani, raia wa Sweden, unaweza kusema huyu alifuata nini kwenye soka - mbona ni pisi kali ambayo inaweza kuwekwa ndani kuliko kuhangaika uwanjani?
Asllani humwambii kitu kuhusu soka amecheza mchezo huo kwa zaidi ya miaka 10 na kupita klabu kadhaa kubwa ikiwemo Manchester City na hadi kufika Real Madrid ya Hispania, na anajua kujitunza na urembo wake ndio maana ukimuona kwa sasa akiwa na miaka 31 hajachakaa.
Sio sawa kuchukulia mchezo wa soka kwa wanawake ni kichaka cha kufanya mambo yasiyofaa kwa jamii, inapaswa kuchukuliwa kama kazi nyingine. Ukiachana na Asllani hizi hapa pisi kali kwenye Ligi ya Wanawake Bara.