Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anasema kwamba hakutakua na majibu mengi licha ya timu hiyo kulazwa 2-1 nyumbani na klabu inayoshikilia mkia Sheffield United .
Kikosi cha Solskjaer kingepanda juu ya jedwali katika ligi ya premia na kutoka nyuma na kuipiku Manchester Coty , iwapo kingeshinda mechi hiyo ya Old Trafford.
Hakuna muda wa kujisamehe , alisema Soskjaer, ambaye timu yake inaelkea katika uwanja wa Emirates kucheza dhidi ya timu ya Arsenal ambayo imemarika kimchezo siku ya jumamosi.
Timu nynegie zimepoteza na kujinasua - pia sisi tumefanikiwa kufanya hilo. Baada ya kucheza na Arsernal, Mechi mbili zinazofuata za United zitakuwa dhidi ya Southmapton na Everton katika uwanja wa Old Trafford- ambapo wameshindwa mechi zote nne msimu huu.
Nataraji kiwango chetu cha mchezo kitaboreka siku ya jumamosi, akiongezea raia huyo wa Norway kufuatia kushindwa kwao.
United imanzisha kampeni ya kushangaza ya kuwania taji la ligi ya uingereza baada ya kucheza mechi 12 bila kushindwa , lakini ikaonesha kiwango cha chini cha mchezo dhidi ya Sheffield ambayo walitarajiwa kuishinda.
Beki wa zamani wa United Rio ferdinand amesema kwamba kikosi cha Solskjaer ambacho kiko katika nafasi ya pili katika jedwali kilikosa fursa kkuonesha ari yake ya kutaka kushinda taji la ligi kwa majirani zao City.
Siku ya Jumanne kikosi cha Pep Guradiola kiliipiku Man United baada ya kuicharaza Wst Brom - 5-0.
Manchester United inafaa kujibu siku inayofuata, nahodha huyo wa zamani wa England alisema akihojiwa na chombo cha michezo cha BT Sport