Klabu ya Tottenham imewasiliana na kiungo wa kati wa PSG na Argentina Angel di Maria kuhusu uhamisho wa kwenda London. Mchezaji huyo wa zamani wa Man United mwenye umri wa miaka 32 anapatikana kwa uhamisho wa bila malipo mwisho wa msimu huu. (L'Equipe via Talksport)
PSG bado inatumai kumsajili kiungo wa kati wa Tottenham na England Dele Alli, 24, kwa mkopo kwa kipindi chote cha msimu kilichosalia . Spurs inafikiria kumsaini kiungo mchezeshaji wa Borussia Monchengladbach na Ujerumani Florian Neuhaus, 23, kama mtu atakeyechukua nafasi yake. (Mirror)
Spurs pia imehusishwa na uhamisho wa beki wa Napoli na Serbia Nikola Maksimovic, 29, ambaye kandarasi yake inakamilika mwisho wa msimu huu. (Spazio Napoli via Sport Witness)