Rais wa Marekani Joe Biden amesema anatarajia taifa la Marekanu hivi karibuni litaanza zoezi la kuchanja watu chanjo ya Corona ambapo litaanza na watu milioni 1.5 kwa siku.
Biden Ikumbukwe awali alitangaza kuwa chanjo milioni 1 zitatolewa kila siku katika siku 100 za kwanza za urais wake.
Lakini vyombo vingine vya habari vilibainisha kuwa Marekani tayari ilikuwa karibu kufikia lengo hilo chini ya utawala wa Trump ambapo ni kuwapa watu chanjo.
Bwana Biden ameweka upya marufuku ambayo yaliwekwa kipindi cha Trump kuhusu marufuku ya kusafiri kutokana na janga la corona siku ya Jumatatu.
Pia Utawala wa Biden Jumatatu uliweka upya marufuku ya kusafiri na kusema kuwa wageni ambao sio Wamarekani kutoka Brazil na na nchi nyingi za Ulaya , pamoja na Uingereza na Ireland hawataruhusiwa kuingia nchini humo.
Mbali na hayo mataifa White House pia imeweka marufuku mpya kwa taifa la Afrika Kusini kutoingia kutokana na uwepo wa virusi aina mpya nchini humo.
Masharti mapya ya kusafiri yamekuja wakati Minnesota ikirekodi maambukizi ya mtu mmoja ya kirusi kipya cha Corona ambaye hivi karibuni alisafiri kwenda Brazil