28 Feb 2021 00:00:00 AM Breaking News
Mukoko amtia Kaze lawamani YangaTetetesi za soka Ulaya Jumanne 09.02.2021: Messi, Lukaku, Ings, Konate, Shoretire, Alaba, ElliottGomez: Tulieni, tupo tayari kwa vitaVikwazo vya kiuchumi Iran havitaondolewaMangungu kuanza na mambo 11 SimbaMastaa Yanga wapewa siku sabaMorrison azidisha utamu SimbaMbunge akumbusha kilio cha Katiba MpyaKaze afunguka ishu ya Yanga kufungiwa kusajiliTanzania Kutopewa Chanjo ya Corona na WHOGomes amtega Mkude SimbaMikataba yote ilioafikiwa siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho UlayaUGANDA: Watu 32 wapoteza maishaKesi ya Iran kuhusu Marekani yasikilizwaChikwende, Lwanga kuonja balaa la Ligi KuuKambi Yanga Dar kibokoTetesi za soka Ulaya Jumatano 03.02.2021: Messi, Neymar, Mbappe, Sancho, Alli, HakimiPisi Kali Ligi Kuu WanawakeBilionea wa Amazon Jeff Bezos ajiuzuluMTV wameingia kwenye 18 za Diamond tena"Kazi ya serikali sio kulisha Watu"- Rais MagufuliMmemsikia Kaze..! kwa mafundi hawa kazi mnayoCristiano Ronaldo achunguzwa kwa kusafiri ili kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mpenzi wake licha ya masharti ya coronaAjali ya treni na Lori la mizigo VingungutiSimba yabeba taji laoWaandamana kupinga sheria ya usalama wa taifa, UfaransaMAGUFULI: Daktari Aliekimbia Hospitali ya Serikali Kwenda Binafsi AfutweRC Mbeya aunda tume kuchunguza kifo cha derevaGomes: Simba yangu... Mtakula nyingiii!Mastaa Yanga tumbo jotoMagufuli "Wivu unavyowakwamisha watanzania"Mamilioni Yanga yaitesa SimbaMkurugenzi WHO kukutana na Mawaziri wa AfrikaNidhamu ya kujilinda imeitoa Stars Waziri Bashungwa: Tutawasaidia Wasafi Tv kufunguliwaMan United kuchuana dhidi ya Arsenal, Everton na Southampton baada ya kulazwa na Sheffield UnitedRais Yoweri Museveni 'Sitaki Kupatanishwa na Wapinzani'Tamko la Rais Magufuli kuhusu magonjwa ya mlipukoHuko Yanga kumekuchaRais Magufuli Awapa Siku 7 Waziri Gwajima na Jafo, Kisa Hichi HapaMorrison ang'ara, Simba ikiua WasudanSerikali Yapiga Marufuku Kuchukua Ardhi Bila Kulipa FidiaKauli ya Farid Musa baada ya kuibeba Taifa Stars “Guinea kazi wanayo” (+video)Serikali kufutia leseni kwa wanaopandisha bei ya mafuta ya kupikiaWallace Karia Apitishwa na FIFATetesi za soka Ulaya Jumatano 27.02.2021: Di Maria, Upamecano, Garcia, Zirkzee, Tarkowski, BentekeAkamatwa Austria na vinyonga 74 kutoka TanzaniaWaziri Mpango: Chukueni Tahadhari Dhidi ya CoronaBarbara: Tulitaka kuialika Yanga Super Cup lakini...Biden aanza na rais wa Urusi: Putin usituingilie hayakuhusuKwa mara ya kwanza mwislamu achaguliwa kama mwanasheria mkuu MarekaniSimba, Al Hilal kamili Super CupRais Magufuli kuzindua shamba la Miti ChatoBiden: Marufuku raia wa Afrika kusini kuingia MarekaniBruno Fernandes: "Iwapo nimechoka, ninapofikia umri wa miaka 30 au 32, sitoweza kucheza''Rais Xi Jinping aonya dhidi ya kuanzisha vita vipya baridiLokosa is RedThe Hammers, hatahivyo wanakabiliwa na ushindani wa kumsajili Lingard, ambaye pia amehusishwa na Aston Villa na Sheffield United. (Express)Trump atuhumiwa kwa kuchochea uasiTetesi za soka Ulaya Jumanne 26.01.2021: Dzeko, Lingard, Alli, Draxler, Mustafi, Veron, GrayBobi Wine ana siku nne za kupinga matokeo mahakamaniJPM Aanika Alichozungumza na Rais wa EthiopiaChelsea imekataa ofa ya West Ham ya kumchukua mlinzi wa Italia, 26, Emerson Palmieri kwa mkopo. (Sunday Mirror)Kikosi kizima TP Mazembe chaanikwa, kutua J5Rais wa Mexico apata maambukizi ya COVID-19BAHANUZI: Maisha yangu Mungu anajuaAjali ya ndege yaua wachezaji wanne na rais wa klabu BrazilTetesi za soka Ulaya Jumatatu 25.01.2021: Odegaard, Lingard, Gilmour, Mbappe, Alaba, ModricMliosambaza Stika za TRA jiandaeni kisaikolojiaMtambo wa mabao Jamie Vardy kufanyiwa operesheniKimbunga Eloise chapiga Msumbiji na kuleta mafurikoUrusi yaishutumu Marekani kwa kuingilia mambo yake ya ndaniKaze aanza na gia mpyaDidier Gomes kocha mpya SimbaLady Jay Dee Awafungukia Wanaopenda Nyimbo za MatusiMwanamuziki Shetta Aachana na MkeweSarpong Abakishwa Kwa Masharti Mazito YangaRC Kunenge apokea msaada wa mifuko 800 ya sarujiMarekani, WHO sasa mambo safiTaifa Stars yakabidhiwa Milioni 60, kila la heri michuano ya CHAN 2021Waziri Mkuu Mongolia ajiuzuluJohn Bocco karudi kuokoa jahazi la Taifa Stars CHAN Viongozi wa Ulaya kutafuta muarubaini wa Corona leoNMB yajipanga kusaidia na kufufuliwa zao la Mkonge nchiniMkude: Simba naombeni msamahaChameleone ashindwa uchaguzi wa umeyaFiston aongeza mzuka Yanga, kuwasili JumamosiTanzia: Mbunge wa CCM Afariki DuniaMajaliwa atoa maagizo haya kwa Wizara ya KilimoRais mpya wa Marekani Joe Biden aanza kazi baada ya kuapishwaKwanini Lampard anastahili muda zaidi Chelsea?Mexico inataka ushirikiano wa Biden kumaliza mgogoro wa wahamiaji mpakaniTanzia: Naibu Kamishna Magereza Afariki DuniaShikhalo: Simba SC itatoboa AfrikaBiden kuapishwa leo, machozi yamtoka kaburini kwa mtoto wake Alichokisema Rais Magufuli Kuhusu Ajira Milioni 8Simba yanasa mbadala wa Mkude MaliBalozi wa Marekani Uganda azuiwa kumuona Bobi WineMarekani! Taharuki ya Mlipuko Eneo la Uapisho wa Joe Biden, Zoezi LaahirishwaOle Gunnar Solskjaer atumia mfano wa Mlima Kilimanjaro kuhamasisha wachezajiPolisi Uganda yathibitisha kumuweka kizuizi cha nyumbani Bobi WineMesut Ozil: Kiungo wa kati wa Arsenal kujiunga na Samatta klabu ya FenerbahceTuisila awatikisa nyota MsimbaziUchaguzi Uganda 2021: Upi mustakabali wa Bobi Wine baada ya kushindwa uchaguzi?Bobi Wine kukimbilia mahakamani kupinga matokeo ya uchaguziChikwende, Mnigeria wamesaini Simba, Morrison mh!Rais Magufuli: Shule ipo Dar Es Salaam wanafunzi wanakaa chini, Mkuu wa Wilaya yupo, Mkuu wa Mkoa yupo, Mkurugenzi wa Ubungo bado anakusanya kodi yupo na Mbunge wa Ubunge yupo tena ni profesa wa Elimu.Jinsi uapisho wa Joe Biden utakavyokuwa tofauti huku ulinzi ukiwa mkali?

Trump atuhumiwa kwa kuchochea uasi

Baraza la Wawakilishi la Bunge la Marekani limewasilisha hati ya mashtaka mbele ya Baraza la Seneti dhidi ya rais wa zamani Donald Trump na kufungua njia ya kuanza kwa shauri la pili la kihistoria.

         USA, Washington I Trump Impeachment

Hati ya mashtaka dhidi ya Donald Trump ikipelekwa mbele ya Baraza la Seneti.

Wawakilishi tisa walioteuliwa kuongoza mchakato huo wamewasilisha shtaka moja pekee linalomtuhumu Trump “kuchochea uasi” baada ya wafuasi wake kuvamia majengo ya Bunge mjini Washington mapema mwezi huu.

Wakitembea kwa mwendo wa polepole wawakilishi hao waliwasilisha hati ya mashtaka mbele ya Baraza la Seneti na kufungua njia ya kuanza kwa shauri la kihistoria kwa kiongozi wa taifa hilo kushtakiwa mara mbili na Bunge.

Mwakilishi wa jimbo la Maryland Jamie Raskin  ndiye alisoma shakta dhidi ya Trump ndani ya ukumbi wa Baraza la Seneti, ambako rais huyo mstaafu bado uungwaji mkono kutoka maseneta wa chama chake cha Republican.

Kuwasilishwa kwa hati hiyo ya mashtaka iliyoidhinishwa na Baraza la Wawakilishi linaloongozwa na chama cha Democrat mnamo Januari 13 kunafungua njia ya kuanza kwa shauri dhidi ya Trump katika wiki ya pili ya mwezi Februari.

Seneti kuongoza shauri na kutoa hukumu

     Ex-US Präsident Donald Trump

Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump

Kiongozi wa walio wengi katika Baraza la Seneti Chuck Schumer amesema wajumbe 100 wa baraza hilo ambalo watafanya kazi kama mahakimu wataapishwa leo Jumanne na tayari wito wa kufika mbele ya baraza umetumwa kwa Bw. Trump.

Wanasiasa wa Democratic na Republican walikubaliana kuchelewesha kwa muda wa wiki mbili kuanza kwa shauri hilo ili kumruhusu Trump kuandaa utetezi wake dhidi ya shtaka linalomkabili la “kuchochea uasi” na kuruhusu Baraza la Seneti kuidhinisha wateule wa nafasi mbalimbali za utawala rais Joe Biden.

Mara hii kesi hiyo itaongozwa na makamu mwenyekiti wa Baraza la Seneti Patrick Leahy kutoka chama cha Democratic ambaye ni seneta mkongwe zaidi badala ya jaji mkuu wa Marekani John Roberts aliyeongoza shauri la kwanza dhidi ya Trump wakati alipokuwa rais.

     USA | Nancy Pelosi hält den Artikel der Amtsenthebung gegen Präsident Donald Trump

Spika wa Baraza la Wawakilishi akionesha hati ya mashtaka aliyoitia saini kabla ya kuwasilishwa kwa Seneti.

Makamu mwenyekiti wa Baraza la Seneti kwa kawaida ndiye huongoza mashtaka dhidi ya kiongozi yeyote asiye rais wa Marekani ambaye shauri lake limewasilishwa mbele ya chombo hicho.

Wakati hayo yakijiri, rais Joe Biden ameonesha kutojishughulisha kabisa na kile kinachoendelea Bungeni dhidi ya mtangulizi wake na shauri linalomkabili.

Wanasiasa wa chama cha Biden wameendelea kutoa wito wa Trump kuwajibishwa kwa kile wanasema alichochea uasi dhidi ya utawala wa Marekani.

Mwakilishi wa chama cha Democratic Jerry Nadler ambaye pia ni mwenyeketi wa kamati ya mahakama ya Baraza la Wawakilishi amesema sasa ni wajibu kwa Baraza la Seneti kufanya kazi yake kwa kumtia hatiani Trump na kumzuia kutowania tena wadhifa utakaomwezesha kusababisha madhara kwa taifa hilo.

Je, wa republican watamwacha solemba Trump?

      Washington | Sturm auf Kapitol | Wikinger-Mann

Wafuasi wa Donald Trump walipovamia majengo ya Bunge mjini Washington.

Wawakilishi 10  kutoka chama cha Republican walijiunga na wenzao wa Democratic kupiga kura za ndiyo za kumfungulia mashtaka Trump kwa kuchochea wafuasi wake kuvamia majengo ya bunge mnamo Januari 6 ili kuzuia kuidhinishwa kwa Biden kufuatia ushindi aloupata kwenye uchaguzi wa Novembva 3 mwaka uliopita.

Watu watano walikufa katika vurumai hiyo ikiwemo afisa mmoja wa polisi na mwandamanaji aliyepigwa risasi na mlinzi wa majengo ya Bunge.

Hii ni mara ya pili kwa Trump kufunguliwa mashtaka. Mwaka mmoja uliopita Bunge lilimshtaki Trump ili kumuondoa madarakani kwa kuishinikiza Ukraine kufanya uchunguzi dhidi ya hasimu wake wa kisiasa wakati huo Joe Biden.

Hata hivyo Baraza la Seneti lililokuwa chini ya udhibiti wa Republican lilimuondolea hatia kiongozi huyo.

Katika shauri la sasa maseneta wa  Republican karibu 17 wanatarajiwa kupiga kura kuunga mkono mashtaka dhidi ya Trump.

Iwapo atapatikana na hatia, Baraza la Seneti linaweza kumpiga marufuku ya kushika tena madaraka, hatua itakayomzuia kuwania tena urais mwaka 2024.