Chelsea imekataa ofa ya West Ham ya kumchukua mlinzi wa Italia, 26, Emerson Palmieri kwa mkopo. (Sunday Mirror)
Bayern Munich imeanza kupiga hatua katika mazungumzo ya mkataba na kiungo wa kati Jamal Musiala, 17, mashabiki wakishuku kuwa huenda Liverpool na Manchester United wanamfuatilia mchezaji huyo wa kimataifa wa England wa Under-21. (Goal)
Burnley wako kifua mbele katika kumsajili mlinzi wa Stoke Nathan Collins, 19 huku Arsenal nayo pia ikimkodolea macho mchezaji huyo. (Sun on Sunday)
Mlinzi wa Ugiriki Sokratis Papastathopoulos, 32, amejipanga kujiunga na Lazio wa Italia baada ya mkataba wake kukatizwa na Arsenal. (Gazzetta dello Sport, via Football Italia)