25 Feb 2021 00:00:00 AM Breaking News
Mukoko amtia Kaze lawamani YangaTetetesi za soka Ulaya Jumanne 09.02.2021: Messi, Lukaku, Ings, Konate, Shoretire, Alaba, ElliottGomez: Tulieni, tupo tayari kwa vitaVikwazo vya kiuchumi Iran havitaondolewaMangungu kuanza na mambo 11 SimbaMastaa Yanga wapewa siku sabaMorrison azidisha utamu SimbaMbunge akumbusha kilio cha Katiba MpyaKaze afunguka ishu ya Yanga kufungiwa kusajiliTanzania Kutopewa Chanjo ya Corona na WHOGomes amtega Mkude SimbaMikataba yote ilioafikiwa siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho UlayaUGANDA: Watu 32 wapoteza maishaKesi ya Iran kuhusu Marekani yasikilizwaChikwende, Lwanga kuonja balaa la Ligi KuuKambi Yanga Dar kibokoTetesi za soka Ulaya Jumatano 03.02.2021: Messi, Neymar, Mbappe, Sancho, Alli, HakimiPisi Kali Ligi Kuu WanawakeBilionea wa Amazon Jeff Bezos ajiuzuluMTV wameingia kwenye 18 za Diamond tena"Kazi ya serikali sio kulisha Watu"- Rais MagufuliMmemsikia Kaze..! kwa mafundi hawa kazi mnayoCristiano Ronaldo achunguzwa kwa kusafiri ili kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mpenzi wake licha ya masharti ya coronaAjali ya treni na Lori la mizigo VingungutiSimba yabeba taji laoWaandamana kupinga sheria ya usalama wa taifa, UfaransaMAGUFULI: Daktari Aliekimbia Hospitali ya Serikali Kwenda Binafsi AfutweRC Mbeya aunda tume kuchunguza kifo cha derevaGomes: Simba yangu... Mtakula nyingiii!Mastaa Yanga tumbo jotoMagufuli "Wivu unavyowakwamisha watanzania"Mamilioni Yanga yaitesa SimbaMkurugenzi WHO kukutana na Mawaziri wa AfrikaNidhamu ya kujilinda imeitoa Stars Waziri Bashungwa: Tutawasaidia Wasafi Tv kufunguliwaMan United kuchuana dhidi ya Arsenal, Everton na Southampton baada ya kulazwa na Sheffield UnitedRais Yoweri Museveni 'Sitaki Kupatanishwa na Wapinzani'Tamko la Rais Magufuli kuhusu magonjwa ya mlipukoHuko Yanga kumekuchaRais Magufuli Awapa Siku 7 Waziri Gwajima na Jafo, Kisa Hichi HapaMorrison ang'ara, Simba ikiua WasudanSerikali Yapiga Marufuku Kuchukua Ardhi Bila Kulipa FidiaKauli ya Farid Musa baada ya kuibeba Taifa Stars “Guinea kazi wanayo” (+video)Serikali kufutia leseni kwa wanaopandisha bei ya mafuta ya kupikiaWallace Karia Apitishwa na FIFATetesi za soka Ulaya Jumatano 27.02.2021: Di Maria, Upamecano, Garcia, Zirkzee, Tarkowski, BentekeAkamatwa Austria na vinyonga 74 kutoka TanzaniaWaziri Mpango: Chukueni Tahadhari Dhidi ya CoronaBarbara: Tulitaka kuialika Yanga Super Cup lakini...Biden aanza na rais wa Urusi: Putin usituingilie hayakuhusuKwa mara ya kwanza mwislamu achaguliwa kama mwanasheria mkuu MarekaniSimba, Al Hilal kamili Super CupRais Magufuli kuzindua shamba la Miti ChatoBiden: Marufuku raia wa Afrika kusini kuingia MarekaniBruno Fernandes: "Iwapo nimechoka, ninapofikia umri wa miaka 30 au 32, sitoweza kucheza''Rais Xi Jinping aonya dhidi ya kuanzisha vita vipya baridiLokosa is RedThe Hammers, hatahivyo wanakabiliwa na ushindani wa kumsajili Lingard, ambaye pia amehusishwa na Aston Villa na Sheffield United. (Express)Trump atuhumiwa kwa kuchochea uasiTetesi za soka Ulaya Jumanne 26.01.2021: Dzeko, Lingard, Alli, Draxler, Mustafi, Veron, GrayBobi Wine ana siku nne za kupinga matokeo mahakamaniJPM Aanika Alichozungumza na Rais wa EthiopiaChelsea imekataa ofa ya West Ham ya kumchukua mlinzi wa Italia, 26, Emerson Palmieri kwa mkopo. (Sunday Mirror)Kikosi kizima TP Mazembe chaanikwa, kutua J5Rais wa Mexico apata maambukizi ya COVID-19BAHANUZI: Maisha yangu Mungu anajuaAjali ya ndege yaua wachezaji wanne na rais wa klabu BrazilTetesi za soka Ulaya Jumatatu 25.01.2021: Odegaard, Lingard, Gilmour, Mbappe, Alaba, ModricMliosambaza Stika za TRA jiandaeni kisaikolojiaMtambo wa mabao Jamie Vardy kufanyiwa operesheniKimbunga Eloise chapiga Msumbiji na kuleta mafurikoUrusi yaishutumu Marekani kwa kuingilia mambo yake ya ndaniKaze aanza na gia mpyaDidier Gomes kocha mpya SimbaLady Jay Dee Awafungukia Wanaopenda Nyimbo za MatusiMwanamuziki Shetta Aachana na MkeweSarpong Abakishwa Kwa Masharti Mazito YangaRC Kunenge apokea msaada wa mifuko 800 ya sarujiMarekani, WHO sasa mambo safiTaifa Stars yakabidhiwa Milioni 60, kila la heri michuano ya CHAN 2021Waziri Mkuu Mongolia ajiuzuluJohn Bocco karudi kuokoa jahazi la Taifa Stars CHAN Viongozi wa Ulaya kutafuta muarubaini wa Corona leoNMB yajipanga kusaidia na kufufuliwa zao la Mkonge nchiniMkude: Simba naombeni msamahaChameleone ashindwa uchaguzi wa umeyaFiston aongeza mzuka Yanga, kuwasili JumamosiTanzia: Mbunge wa CCM Afariki DuniaMajaliwa atoa maagizo haya kwa Wizara ya KilimoRais mpya wa Marekani Joe Biden aanza kazi baada ya kuapishwaKwanini Lampard anastahili muda zaidi Chelsea?Mexico inataka ushirikiano wa Biden kumaliza mgogoro wa wahamiaji mpakaniTanzia: Naibu Kamishna Magereza Afariki DuniaShikhalo: Simba SC itatoboa AfrikaBiden kuapishwa leo, machozi yamtoka kaburini kwa mtoto wake Alichokisema Rais Magufuli Kuhusu Ajira Milioni 8Simba yanasa mbadala wa Mkude MaliBalozi wa Marekani Uganda azuiwa kumuona Bobi WineMarekani! Taharuki ya Mlipuko Eneo la Uapisho wa Joe Biden, Zoezi LaahirishwaOle Gunnar Solskjaer atumia mfano wa Mlima Kilimanjaro kuhamasisha wachezajiPolisi Uganda yathibitisha kumuweka kizuizi cha nyumbani Bobi WineMesut Ozil: Kiungo wa kati wa Arsenal kujiunga na Samatta klabu ya FenerbahceTuisila awatikisa nyota MsimbaziUchaguzi Uganda 2021: Upi mustakabali wa Bobi Wine baada ya kushindwa uchaguzi?Bobi Wine kukimbilia mahakamani kupinga matokeo ya uchaguziChikwende, Mnigeria wamesaini Simba, Morrison mh!Rais Magufuli: Shule ipo Dar Es Salaam wanafunzi wanakaa chini, Mkuu wa Wilaya yupo, Mkuu wa Mkoa yupo, Mkurugenzi wa Ubungo bado anakusanya kodi yupo na Mbunge wa Ubunge yupo tena ni profesa wa Elimu.Jinsi uapisho wa Joe Biden utakavyokuwa tofauti huku ulinzi ukiwa mkali?

NMB yajipanga kusaidia na kufufuliwa zao la Mkonge nchini

Benki ya NMB imesema kuwa itahakikisha inaendelea kutoa huduma za kifedha kwa kushirikiana na wadau
mbalimbali katika kufufua zao la Mkonge na kuboresha uchumi wa wakulima wa zao hilo nchini. Hatua hiyo inakuja baada ya serikali kuanza mikakati ya kuhakikisha zao hilo linafufuliwa na kuwanufaisha wakulima na taifa kwa ujumla kama ambvyo ilivyokuwa miaka ya nyuma.


Akiongea mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wa kikao cha wadau wa Mkonge kilichofanyika jana
Mkoani Tanga, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi  na Biashara wa Benki hiyo – Filbert Mponzi, alisema kuwa NMB itaendeleza jitihada za kufufua zao hilo ambazo imezianza.

Alisema kuwa tangu serikali imeanza kulifufua zao hilo Benki hiyo imekuwa ikitoa ushirikiano ambapo imetoa zaidi ya Bilioni 1 kwa ajili ya ununuzi wa matrekta 11 na trela 22 vifaa ambavyo vitapunguza gharama ya uendeshaji na kuongeza tija na pato la wakulima wadogo wa mkonge.Aidha aliongeza kuwa Benki hiyo imeendelea kutoa mikopo ya pembejeo na uendelezaji wa mashamba ya Mkonge kwa wakulima wadogo, kati na wakubwa ili kuongeza uzalishaji na mapato ambapo zaidi ya shilingi bilioni 6 zimeshatolewa kwa wakulima wa mkonge.

Alisema kuwa NMB imefanikisha kufungua akaunti kwa wakulima zaidi ya 1,500 ambapo akaunti hizo zinajumuisha wakulima mmoja mmoja na wale wanaozalisha kupitia Vyama vya Msingi.

“Uwepo wa akaunti hizi unajenga utamaduni wa wakulima kutumia huduma za benki kwa usalama wa fedha

zao na mazingira sahihi katika kupata huduma zaidi ya kifedha ikiwemo Mikopo” alisema Mponzi.

Mheshimiwa Waziri Mkuu ili kuendelea kuwajengea uwezo wakulima wadogo na kupata mitaji NMB kupitia
taasisi kanzu ya NMB Foundation inaendelea kutoa mafunzo kwa wakulima kupitia vyama vya vya msingi na
kikundi ili kuimarisha utendaji na kuongeza soko," alifafanua.

Mponzi alibainisha kuwa Benki ya NMB itaendeleza jitihada hizo, ikiwemo kutoa mikopo mikubwa, midogo na ya kati ili kuhakikisha wakulima wa zao wanazlisha kwa tija.

“NMB tutaendelea mikopo katika ngazi zote za uzalishaji wa zao la mkonge, ikijumuisha mikopo ya muda mfupi na muda wa kati (yaani uwekezaji). Mikopo hii inajumisha pembejeo, upanuzi na miundo mbinu ya mashamba, matrekta, mashine za uchakataji wa mkonge, viwanda vya mkonge pamoja na huduma mbalimbali katika sekta,” alisema.

Akizungumza katika kikao hicho cha wadau wa zao la Mkonge, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema kuwa mpaka kufikia mwaka 2025 Tanzania inatarajia kuzalisha tani 120,000 za Mkonge kwa mwaka. Majaliwa alisema kuwa zao la Mkonge ni miongoni mwa mazao ya biashara hapa nchini ambayo mikakati yake ilitekelezwa vizuri itawezesha serikali kupata fedha za kigeni lakini pia kukuza pato la mwananchi mmoja mmoja.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe alisema kuwa kwa sasa Wizara tayari imeshatenga shilingi Bilioni 175 kwa ajili ya kufanya utafiti ili kuzalisha mbegu bora na zenye gharama nafuu.
Bashe alisema kuwa Wizara imeweza kuandaa utaratibu wa hati ya dhamana (LC) utakaowezesha wakulima
wadogo kuchukua mkopo kwenye taasisi za fedha kwa riba ya asilimia mbili tu.