Joe Biden na Kamala Harris wataapishwa madaraka mapya Januari 20
Joe Biden anatarajiwa kuapishwa kuwa rais wa 46 wa Marekani.
Imejulikana kwa muda mrefu mipango ya shughuli hii ambayo ilipangwa kufanyika Januari 20. ambayo itakuwa tofauti kutokana na masharti dhidi ya virusi vya corona.
Lakini kuna masuala matatu ya ziada ambayo yameongezewa kutarajiwa kutokea:
Janga la corona ndio suala la hatari kubwa nchini Marekani, huku kukiwa na rekodi mpya ya maambukizi ya virusi vya corona na vifo.
Mgogoro wa kisiasa baada ya wafuasi wa Trump kuvamiwa kwa jengo la bunge Januari 06, rais Trump anatarajiwa kushitakiwa kutokana na tukio hilo na kukataa kukubali matokeo ya uchaguzi ya Novemba 3.
Tahadhari kutoka vyombo vya usalama juu ya tishio linaloweza kutokea la maandamano au ghasia katika siku hiyo ya uapisho.
Kukabidhiana kwa madaraka kama ilivyokuwa jadi nchini Marekani kunatarajiwa kuhudhuriwa na chama cha democratic kwa wingi.
Wakati huu mambo yanaonekana kuwa tofauti.
Shughuli za kuapishwa zina maana gani?
Kihistoria, sherehe za kuapishwa huwa ni maadhimisho ya demokrasia nchini Marekani.
Kikubwa ambacho kinahitajika ni kwa rais mteule kusema kiapo chake : "Ninaapa kuwa mwaminifu kwa kuitumikia ofisi ya rais kwa uwezo wangu wote, nitailinda na kuitetea katika ya Marekani." .
Nitakapo zungumza maneno haya , Biden atachukua nafasi yake kama rais wa 46 wa Marekani na zoezi la kuapishwa litakuwa limemalizika, na sherehe kufuatia.
Kamala Harris atakuwa makamu wa rais mara atakapoapa , na makamu huuwa anakula kiapo muda mfupi kabla ya rais kuapishwa.
Wakati gani maadhimisho hufanyika
Kisheria ni siku ya Januari 20.
Mwaka huu, hotuba itatolewa majira ya saa tano na nusu (16:30 GMT), Joe Biden na Kamala Harris kuchukua ofisi saa sita mchana.
Baadae siku hiyo, Biden atahamia White House, na kukaa kwa miaka minne.
Ronald Reagan akiapishwa
Kuapishwa huwa si lazima ufanyike Januari . Katiba inasema Machi 4 ndio kiongozi mpya anakabidhiwa ofisi na kula kiapo.
Kuchaguliwa kwa tarehe huwa ni miezi minne kabla ya uchaguzi mkuu wa Novemba, kwa kuwa ilikuwa inachukua muda mrefu kuhesabu kura.
Kukua kwa teknolojia kumerahisisha mambo na kufanya zoezi la kuhesabu kura kuwa la haraka na hivyo kubadilisha muda wa makabidhiano ya madaraka ukabadilishwa na kuwa Januari 20.
Usalama utakuwaje?
Siku ya kuapishwa kwa rais , ulinzi huwa ni mkali.
Na kwa wakati huu ulinzi utaimarishwa zaidi kutokana na tukio la wafuasi wa Trump kuvamia jengo la bunge Januari 6.
FBI imetoa angalizo dhidi ya maandamano yanayoweza kutokea capitols na Washington DC siku chache kuelekea maadhimisho hayo, hivyo ulinzi kuimarishwa na sekta kubwa kufungwa.
Baadhi ya wafuasi wa Trump waliovamia jengo la bunge
Ijumaa, jeshi lilitangaza kuongeza wanajeshi 25,000 wakati wa kuapishwa kwa Biden, wengine 4,000 zaidi waliagizwa Alhamisi.
Je Trump atahudhuria sherehe hizo?
Kwa kawaida rais anayetoka anapaswa kuepo na kushuhudia mrithi wake akila kiapo.
Barack Obama alihudhuria uapisho wa Donald Trump.
Mwaka huu , hali itakuwa tofauti rais anayeondoka madarakani hatadhuria uapisho wa rais mpya.
"Kwa kila mtu anayeuliza, sitahudhuria sherehe za uapisho Januari 20, " Trump aliandika katika twitter yake Januari 8.
Trump alitangaza kutohudhuria uapisho wa Joe Biden.
Ujumbe huo ulitolewa muda mfupi mara baada ya rais kutakiwa kukabidhi madaraka kwa serikai mpya kwa kufuata utaratibu.
Zaidi ya watu 68,000 wamesema Facebook kuwa watafuatilia uapisho huo mtandaoni ili kuonesha jinsi wanavyomuuga mkono.
Ingawa makamu wa rais Mike Pence, alisema atahudhura shughuli hiyo.
Mike Pence, makamu wa rais wa Trump ataudhuria sherehe hizo
Wakati Trump alipoapishwa mnamo mwaka 2017, Hillary Clinton alihudhuria kwenye sherehe hizo na mumewe, Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton, miezi miwili tu baada ya kushindwa kwake uchaguzi na kampeni ngumu dhidi ya Trump.
Ni marais watatu tu - John Adams, John Quincy Adams na Andrew Johnson - waliamua kutoshiriki uzinduzi wa warithi wao, jambo ambalo hakuna rais aliyefanya katika karne iliyopita.
Je! Janga litaathirije sherehe ya mwaka huu?
Katika hali ya kawaida, Washington DC ingeona mamia ya maelfu ya watu wakimiminika kushuhudia uzinduzi huo.
Barack Obama alipoapishwa mwaka 2009.
Karibu wageni milioni mbili walifika katika mji mkuu wa Marekani wakati Rais Obama alipokuwa anaapishwa mnamo 2009.
Lakini mwaka huu, sherehe itakuwa "mdogo sana," kulingana na timu ya Biden, ambayo imewataka Wamarekani kuepuka kusafiri kwenda mji mkuu.
Biden na Harris wataendelea kuapishwa mbele ya Capitol, katika eneo linalotazama eneo maarufu la National Mall esplanade (utamaduni ulioanza na Rais Ronald Reagan mnamo 1981).
Hapo awali, kulikuwa na tiketi hadi 200,000 zilizopatikana kuhudhuria sherehe hiyo rasmi lakini mwaka huu, maambukizo yanaendelea kuongezeka nchini Marekani, na tiketi karibu 1,000 tu ndio zitapatikana.
Mwaka huu bado kutakuwa na sherehe za jadi , lakini badala ya gwaride la kawaida chini ya Pennsylvania Avenue kwenda Ikulu, waandaaji wanasema wataandaa "gwaride mtandaoni."
Ni wasanii gani wataalikwa?
Katika miaka ya hivi karibuni, marais watakaokuja wameongeza wasanii wapendwa zaidi nchini kwenye programu ya siku hiyo. Licha ya janga hilo, mwaka huu hakutakuwa tofauti.
Biden na Harris watatumbuizwa na Lady Gaga
Lady Gaga alimfanyia kampeni Biden na atakuepo kwenye uapisho
Lady Gaga ataimba wimbo wataifa na Jennifer Lopez ataimba wakati wa onyesho la muziki la sherehe hiyo.
Baada ya kuapishwa kwa Biden, muigizaji Tom Hanks atakuwa mwenyeji wa kipindi cha televisheni cha kwanza cha dakika 90, mbadala unaofaa wa janga la sherehe ambazo kawaida hufanyika kibinafsi.
Itashirikisha Jon Bon Jovi, Demi Lovato na Justin Timberlake, na itaruka hewani kwenye mitandao yote ya Marekani na majukwaa, isipokuwa Fox News, mtandao uliomsaidia Trump wakati wa urais wake.
Mnamo 2009, Aretha Franklin aliimba wakati wa uzinduzi wa Barack Obama, akiimba wimbo wa "My Country 'Tis of Thee." Beyonce pia alikuwepo, akiimba "At Last".
Katika kuapishwa kwake kwa pili mnamo 2013, Obama aliuliza Kelly Clarkson na Jennifer Hudson wafanye heshima. Beyonce alirudi tena, wakati huu kuimba wimbo wa taifa .
Beyonce alitumbuiza mara zote mbili za kuapishwa kwa Barack Obama