Kocha wa Barcelona Ronald Koeman amesema kuwa "ana imani lakini hana uhakika" kama mshambuliaji wa Argentina, 33, Lionel Messi atasalia kwenye klabu hiyo msimu huu. (Athletic - subscription required)
Mkataba wa Messi wa pauni milioni 492 na Barcelona ambao unakamilika mwisho wa msimu, unajumuisha kipengee ambacho kinamruhusu kuondoka bila masharti yoyote ikiwa Catalonia itapata uhuru wake. (El Mundo, via Mail)
Mshambuliaji wa Brazil Neymar, 28, atasaini mkataba mpya wa miaka minne na mabingwa wa Ufaransa Paris St-Germain. (Goal)