Mshambuliaji wa Juventus Cristiano Ronaldo anachunguzwa na maafisa wa polisi wa Itali kuhusu safari aliokwenda ili kusherehekea siku ya kuzaliwa na mpenzi wake.
Anatuhumiwa kwa kuvunja masharti ya Covid -19 kwa kusafiri kati ya jimbo la Piedmont na Valle d'Aosta.
Picha zilizochapishwa na baadaye kuondolewa mtandaoni zinawaonesha wawili hao wakiwa katika hoteli moja siku ambayo Georgina Rodriguez alisherehekea kua na umri wa miaka 27.
Italy imeshuhudia mamia ya vifo na maelfu ya maambukizi mapya kila siku.
Taifa hilo liliathiriwa vibaya mapema wakati wa mlipuko huo mwaka uliopoita na sasa liko katika mzozo wa ksiasa baada ya kushindwa kupunguza idadi maambukizi katika wimbi la pili la maradhi hayo.
Maafisa wa polsi wa Valle d'Aosta wanasema kwamba wanawachunguza wapenzi hao kuhusu safari hiyo ya mgahawa wa Courmayeur ski
Chini ya sheria zilizopo nchini Itali, safari kati ya maeneo yenye maambukizi ya Corona zimepigwa marufuku isipokuwa iwapo ni ziara ya kikazi ama kwenda nyumbani
Ripoti nchini Itali zinadai kwamba wawili hao walisafiri siku ya Jumanne na kusalia katika mgahawa huo usiku kucha kabla ya kurudi Turin, nyumbani kwa klabu ya Serie A Juventus siku ya Jumatano.
Rodriguez, ambaye ni mwanamitindo , baadaye alichapisha picha ya yeye na Ronaldo wakisherehekea nyumbani kwao na familia
Endapo watapatikana wamekiuka sheria huenda wote wakapigwa faini.
Utata huo unajiri miezi kadhaa baada ya Ronald kuabukizwa corona . Wakati huo alikosolewa na waziri wa Michezo nchini Itali kwa kwenda Portugal ili kushiriki katika mechi ya kimataifa muda mfupi kabla ya kupatikana na maambukizi ya ugonjwa huo.
Vincenzo Spadafora alimtaja Ronaldo kama mtu mwenye 'kiburi' na asiye na 'heshima' na kumshutumu kwa kukiuka itifaki za maradhi ya Corona kwa kuwacha hoteli ya timu yake na kusafiri baada ya kuripoti maambukizi.
Hathivyo mchezaji huyo amekana kufanya makosa.