MICHUANO ya Simba Super Cup kwa msimu wa kwanza imemaliza leo Jumapili kwa Simba kuibuka mabingwa wa mashindano hayo yaliyofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Simba ndio waliandaa michuano hiyo mifupi na kuzialika klabu za Al Hilal ya Sudan na TP Mazembe ya DR Congo ambapo kila timu imecheza mechi mbili.
Simba imekuwa mabingwa baada ya kutoa suluhu kwenye mchezo wa mwisho wa michuano hiyo na kujikusanyia alama nne ambazo ni zaidi ya zile tatu za Al Hilal na moja ya TP Mazembe.|
Mechi ya ufunguzi Simba alishinda bao 4-1 mbele ya Al Hilal, mchezo uliofuata Hilal wakaibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Mazembe na mchezo wa mwisho ni huu uliomalizika dakika chache zilizopita kwa sare tasa kati ya Simba na TP Mazembe.