Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Innocent Lugha Bashungwa ameeleza kuhusu kufungiwa kwa Vyombo vya Habari na Wasanii na kuzungumzia kuhusu Wasafi Tv.
Akiongea katika kipindi cha Clouds Fm Waziri ameeleza haya.
“Kama Wizara jukumu letu la kwanza ni kusimamia nidhamu, inapotokea chombo chochote cha habari au msanii kufungiwa inakuwa wamefikia hatua ambayo hata mimi kama mzazi nimefikia mwisho ndio maana hata lilipotokea la juzi (WasafiTV) tumekaa kujadili tunawasaidia vipi na ninaamini tutawasaidia”
“Tunapanga kujenga Sports Arena Dodoma na itakuwa ni multipurpose na itakuwa inahusisha michezo mbalimbali, Arena hiyo imepewa jina la SPORTS ARENA CHANGAMANI”