Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli amesema licha ya uwepo wa magonjwa ya mlipuko kama Corona lakini watanzania hatutajifungia.
Rais Magufuli ameyasema hayo Januari 27, 2021 alipokuwa akizindua shamba la miti la Chato lililopo wilayani Chato mkoani Geita.
''Nchi nyingi wamejifungia ndani, Watanzania hatujajifungia na hatutegemei kujifungia na wala sitegemei kutangaza kwamba tunajifungia ndani kwa sababu Mungu wetu yupo", amesema Rais Magufuli.
Aidha katika kuchukua tahadhari juu ya magonjwa ya mlipuko, Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli amesema watu waendelee kujifukiza na kuomba mungu pamoja na kufanya mazoezi.